Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova amekanusha kupiga marufuku maandamano ya kumsindikiza Lowassa Kuchukua fomu ya kugombea urais ofisi za tume ya taifa ya uchaguzi.
Kova amesema kuwa maandamano wanayo yatambua ni yale yanayo anzia ofisi za CHADEMA kwenda NEC,lakini ya kutoka Nec kwenda makao makuu ya CUF Buguruni hawayatambui.
Katika Hatua nyingine, Mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Mbowe amesema hawana taarifa yoyote ya zuio la maandamano toka jeshi la polisi.
Mbowe amesisitiza kuwa maandamano ya kumsindikiza Lowassa NEC yako palepale na amewataka wapenzi na wafuasi wa UKAWA wasiogope.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni